Mr Afya Nzuri
Karibu kwa Dondoo za afya, Ushauri, Matibabu, Vipimo, Maswali kiafya,Tiba lishe, tunazingatia siri.
03/02/2024
✴️ ASILIMIA 92.3 YA WATANZANIA WANASUMBULIWA NA MARADHI YANAYO JIRUDIA MARA KWA MARA, HATA BAADA YA KUPATA TIBA✴️
🈴 HIYO HUSABABISHWA NA:-
1. VIPIMO DHAIFU VYA KIUTAFITI (50%)
👉 Vipimo Vinavyotumika Kutotosheleza.
2. MATIBABU YASIYO SAHIHI (25%)
👉 Kutokana Na Vipimo Kutojitosheleza, Matibabu Nayo Yanakuwa Ya Kupoza Maradhi Na Siyo Kutibu Kabisa.
3. MFUMO WA MAISHA (25%)
👉 Aina Ya Shughuli Za Kila Siku Na Vyakula Unavyokula Kusaidia Mwili Kuzalisha Kinga, Kutunza Na Kujenga Afya Yako.
🙂 USIJALI TENA KATIKA HILO
Mr Afya Nzuri Imekuletea Suluhisho La Afya YAKO Kwa Kukupatia:-
✓VIPIMO THABITI VYA KIUTAFITI.
👉 Vipimo Vya Mwili Mzima Kwa OFA Ya 20,000/=tu.
✓ MATIBABU SAHIHI .
👉Tiba Inayoondoa Kuanzia Chanzo Cha Tatizo Na Kufanya Ugonjwa Usijirudie Tena.
✓ NJIA SAHIHI YA MAISHA.
👉 Virutubisho Sahihi Vya Kutumia Kuboresha Afya Yako, Kutokana Na Mfumo Wako Wa Maisha Na Shughuli Zako Za Kila Siku .
📲+255-750-428-705
01/02/2024
🧖🏻♀️ *KUKOMA KWA HEDHI KWA MABINTI WADOGO:*
🧑💻Shida Hii Sasa Tuichambue Kwa kina...
Katika Kizazi Cha sasa Jamii zimekuwa na Changamoto kubwa Katika mpangilio wa hedhi Kwa MABINTI na kutoeleweka Nini chanzo au hali Hii inatokana na Nini ndani ya Umri mdogo
👁️👁️Tuangalie Sababu kadhaa zinazoleta Shida Hii Katika Umri wa Mabinti:-
*🤦🏻♀️Upungufu wa uwezo wa Ovari kwa mwanamke (POI)*
Kukoma hedhi yoyote ambayo hutokea kabla ya umri wa miaka 40 inahusishwa na hali hii ya kupungua uwezo wa ovari za mwanamke.
Mara nyingi hakuna sababu maalum ya hii. Wanawake walio na POI hawapati dalili za kukoma hedhi hadi wafikishe miaka hamsini.
Upungufu wa uwezo wa Ovari kwa mwanamke (POI)
Kukoma hedhi yoyote ambayo hutokea kabla ya umri wa miaka 40 inahusishwa na hali hii ya kupungua uwezo wa ovari za mwanamke.
Mara nyingi hakuna sababu maalum ya hii. Wanawake walio na POI hawapati dalili za kukoma hedhi hadi wafikishe miaka hamsini.
Hii Shida ya POI Kwa mabinti pia inaweza kusababishwa na kingamwili, matatizo ya kromosomu, au upasuaji wa tumbo na ovari.
Pamoja na athari za kimwili za aina hii ya ugonjwa, athari za akili pia zinaweza kuwa hatari sana
Hapa ovari zake huacha kufanya kazi. Pia, mwili wake hauwezi kuzalisha homoni za estrojeni na progesterone za kutosha.
📌Homoni hizi aina mbili ndizo hudhibiti mzunguko wa hedhi katika mwili. Upungufu wa homoni hizi huweza kuathiri mwili wa binti, Hata hivyo Ikiwa ni Upungufu wa homoni hizi Katika Mwili wa Binti basi Dalili huanza Mapema Kujitokeza Sio hali ya Ghafla sana.
*🤦🏻♀️Athari za pombe, Sigara Madawa ya Kulevya na ngono mwilini*
Hii inazungumziwa Kwa Sababu ya Kuathiri Vichocheo Katika Mwili wa Binti ni Vema sana kuepuka Mambo haya ya Matumizi ya Pombe, Sigara na Madawa ya Kulevya
Pia Ngono Katika Umri mdogo yaweza Kuchochea Shida Hii Kwa kuwa anakuwa amewahi ngono mapema sana Mwili wa Binti unakuwa bado haujajiandaa Vema Katika Kukabiliana na utengenezaji Mzuri katika Mfumo wa Siku za hedhi zake.
*Itaendelea...*
*Dr Afya Nzuri * 🌍
Asante Kwa Kuchagua Jukwaa hili na
🌍Kwa Dawa zetu, Tiba za Magonjwa Mbali Mbali, Ushauri na Msaada
Usisite Kuzungumza Ndani ya Kikundi husika au Mazungumzo ya Faragha
Namba ni
🤳+2550750428705
*Karibu sana*
01/02/2024
*SARATANI YA SHINGO YA UZAZI*
Kuna aina mbili za seli kwenye shingo ya kizazi (cervix) ambazo ni
*squamous cells* na
*glandular cells* , hivo saratani ambayo huanzia kwenye seli za squamous huitwa “ *squamous cell carcinoma* ” na saratani inayoanzia kwenye seli za glandular huitwa “ *adenocarcinoma* ”. Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba Saratani inapoanza huwa ni vigumu sana kuigundua kwani haioneshi dalili zozote, hivo unaweza usigundue mpaka pale saratani imefikia hatua mbaya Zaidi, pale ambapo dalili k**a kutokwa na majimaji au maumivu wakati wa tendo la ndoa. Seli za kansa ya shingo ya kizazi hukua taratibu na huchukua miaka michache kwa seli za kawaida kubadilika kuwa seli za kansa, ndio maana inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua mapema.
*📡CHANZO & SABABU ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI*
Wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu huwa na kisababishi kimoja au zaidi kinachojulikana ambacho huongeza hatari ya kuupata. Vifuatavyo ni visababishi vikuu:
1️⃣Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16)
2️⃣Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
3️⃣Maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus)
4️⃣Maambukizo ya magonjwa ya zinaa
5️⃣Umri zaidi ya miaka 30
6️⃣Upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI)
7️⃣Uvutaji wa sigara
8️⃣Kupata mimba katika umri mdogo
9️⃣Idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara
🔟Hali duni ya kiuchumi
1️⃣1️⃣Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye mkewe alikufa kwa saratani ya shingo ya kizazi
1️⃣2️⃣Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa
1️⃣3️⃣Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia
1️⃣4️⃣Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo na kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja ni visababishi vinavyoongoza.
1️⃣5️⃣Pia maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus), huchangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha ugonjwa huu.
*DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.*
Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.
➡️Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (va**na) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
➡️Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
➡️Maumivu wakati wa kujamiana.
*Dalili za saratani iliyosambaa ni k**a zifuatavyo*
➡️Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
➡️Kupungua kwa hamu ya kula
➡️Kupungua uzito
➡️Kuhisi uchovu
➡️Maumivu ya nyonga
➡️Maumivu kwenye mgongo
➡️Maumivu ya mguu
➡️Mguu mmoja kuvimba au Yote
➡️Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke
➡️Kuvunjika mifupa (bone fractures)
➡️Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.
*🌏MAKUNDI YA SARATANI YA KIZAZI*
Saratani ya shingo ya kizazi imegawanywa katika makundi kulingana na TNM ama FGO (Classification) k**a ifuatavyo;
*🧑💻🌏Stage I*
Saratani iliyo kwenye chembechembe au seli za aina ya epithelium lakini haifiki kwenye nyama za ndani za shingo ya kizazi,
*🧑💻🌏Stage I*
Saratani iliyopo kwenye shingo ya kizazi,
*🧑💻🌏Stage II*
Saratani iliyosambaa hadi kwenye tupu ya mwanamke sehemu ya juu kwa 2/3,
*🧑💻🌏Stage III*
Saratani iliyosambaa hadi kwenye ukuta wa nyonga na sehemu ya chini ya uke kwa 1/3, Hii inaleta madhara katika figo,
*🧑💻🌏Stage IV*
Saratani iliyosambaa hadi nje ya tupu ya mwanamke na pia husambaa hadi kwenye sehemu nyingine za mwili k**a mapafu, figo, mifupa nk.
*❓WATU GANI WAPO KWENYE HATARI KUBWA YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.*
Kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo unaweza kuzifanyia kazi na kuunguza hatari ya kupata saratani hii, japo pia kuna njia ambazo ni vigumu kuepuka za ziko nje ya uwezo wetu k**a vile uwepo wa saratani hii katika historia ya familia yako mfano k**a mama ama dada yako aliwahi kupata saratani hii basi unaweza kuwa kwnye hatari kubwa nawe kupata. Makundi mengine ni k**a
💁Wanawake kwenye umri kati ya miaka 20-50 wapo kwenye hatari Zaidi
Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
💁Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongzeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi.
💁Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata saratani hii.
*MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.*
Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, na inahusisha
🤷Kufanyiwa upasuaji na kuondoa mfuko wa mimba (uterus) na viungo vingine k**a ovari na mirija ya uzazi
Matibabu kwa kutumia dawa kali(chemotherapy) ili kuongeza muda wa kuishi
Matibabu kwa njia ya mionzi ili kuua seli za saratani.
🤷Kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu mara kwa mara.
🤷Kupata chanjo dhidi ya virusi vya HPV kabla ya kuanza vitendo vya ngono.
Kupata elimu sahihi kuhusu ugonjwa huu.
🤷Kujiepusha na mambo hatarishi yanayosababisha kuupata ugonjwa huu.
🤷Ugunduzi wa mapema katika hatua za awali za ugonjwa huu na kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati.
*🧑💻MAMBO 10 UNAYOWEZA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI*
🙏Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote pia Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
🙏Kuwa na mpenzi mmoja, Usichangie mapenzi na watu wengi
🙏Kula chakula chenye afya hasa vyakula asilia
Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
🙏Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
🙏Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
🙏Epuka matumizi ya Dawa za uzazi wa mpango zenye madhara
🙏Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
🙏Punguza unywaji wa pombe
🙏Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.
*TIBA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI*
✍️Tiba ya saratani hii inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo.
💉💉Kuna Tiba ya kuchoma (cauterization),
💉💊Tiba ya dawa (Chemotherapy),
🔎🔭Tiba ya mionzi (radiation therapy),
💉🔭Tiba ya upasuaji (surgical treatment),
💊💊Tiba Kwa kutumia Dawa za kisasa katika mpago wa upandikizaji (Stempcells)
✍️🤷Matatizo ya uzazi yanaweza kutibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za saratatani ya shingo ya kizazi na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.
*DAWA*
*Dr Afya Nzuri
🧑💻Tunazo Dawa za kisasa Maalumu kwa kutibu ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni Teknolojia ya Juu Duniani Katika matibabu bila kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa.
Dawa hizi hutibu kabisa Saratani aina yoyote ile
Na Muda wa Dozi ni kuanzia miezi mitatu(2) hadi miezi minne(4) kulingana na Hatua (Stages) pia Muda wa tatizo, Tatizo halirudi tena maana huondoa kile chanzo pamoja na ugonjwa sio kutuliza maumivu, ukianza kutumia baada ya wiki mbili huonesha mabadiliko.
🧑🏻⚕️Wasiliana nas
Kwa Mazungumzo yako ya Faragha Tumia namba...
👇
🤳+0750428705
01/02/2024
SIO DAWA ZOTE ZIPO KWENYE MADUKA YA MADAWA
1 - Mazoezi ni dawa.
2 - Kufunga ni dawa.
3 - Chakula cha asili ni dawa.
4 - Kicheko ni dawa.
5 - Mboga na matunda ni dawa.
6 - Usingizi ni dawa.
7 - Mwanga wa jua ni dawa.
8 - Kuwapenda wengine ni dawa
9 - Kujipenda ni dawa.
10 - Shukrani ni dawa.
11 - Kuacha kosa ni dawa.
12 - Kutafakari ni dawa.
13 - Kusoma na kujifunza Neno la Mungu ni dawa.
14 - Kula vizuri, kwa wakati na bila ziada ni dawa.
15 - Fikra sahihi ni dawa.
16 - Kumtegemea Mungu ni dawa
17 - Marafiki wazuri ni dawa.
18 -. Kujisamehe na kusamehe wengine ni dawa.
19 - Kunywa maji mengi ni dawa.
20 Moyo wenye amani ni Dawa
🙏🙏🙏🏽
25/01/2024
*UGONJWA WA BAWASIRI ~CHANZO, DALILI & TIBA*
*UTANGULIZI*
-Bawasiri ni uvimbe wa mishipa iliyo ndani na karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa au kwenye puru ya chini. Bawasiri huasiri mfumo wa mmeng’enyo hasa utumbo mkubwa chini mwishoni. Karibu asilimia 50 ya watu wazima hupata dalili za bawasiri na umri wa kawaida na hadi miaka 50 na zaidi.
*AINA ZA BAWASIRI*
-Bawasiri inaweza kuwa ya ndani au nje. Bawasiri za ndani hua ndani ya sehemu ya haja kubwa au puru. Bawasiri ya nje huendelea nje ya sehemu ya kutolea haja kubwa. Bawasiri pia hujulikana k**a Marundo.
Bawasiri ya nje ni ya kawaida na yenye shida zaidi. Bawasiri husababisha maumivu, kuwasha hasa sehemu ya haja kubwa, na ugumu wa kukaa. Kwa bahati nzuri, zinatibika.
*CHANZO CHA UGONJWA WA BAWASIRI*
Bawasiri hutokea pindi mishipa inayozunguka sehemu ya kutolea haja kubwa kwa ndani kwenye kuta zake kuumia au kukandamizwa kwa kushuka chini na kuvimba.
Bawasiri inaweza kukuza kutoka kwa shinikizo lililoongezeka kwenye puru ya chini kwa sababu ya:
*1* . Kuwa na Kinyesi kigumu (Constipation)
*2* . Kuketi kwa muda mrefu kwenye choo
*3* . Kuharisha (Kuhara) mara kwa mara
*4* . Kuvimbiwa
*5* . Kuwa mnene au mzito
*6* . Kuwa mjamzito
*7* . Kuingiliwa nyuma kimaumbile
*8* . Kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi
*9* . Kuinua/Kunyanyua vitu vizito mara kwa mara
*10* . Kunyoosha wakati wa haja kubwa
*🧑💻🌏DALILI ZA UGONJWA WA BAWASIRI*
Ishara na dalili za bawasiri kawaida hutegemea aina ya Bawasiri
*BAWASIRI YA NJE*
Hizi ziko chini na nje ya ngozi karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa. Ishara na dalili zinaweza kujumuisha:
*1* . Kuwasha katika maeneo yaliyozunguka sehemu ya haja kubwa
*2* . Maumivu au usumbufu
*3* . Kuvimba kuzunguka sehemu ya kutolea haja kubwa
*4* . Mara nyingine yaweza Kuvujadamu au k**a michubuko
*5* . Kutokwa na kinyama baada ya kwenda haja.
*BAWASIRI YA NDANI*
Bawasiri ya ndani iko ndani ya sehemu ya kutolea haja. Kawaida huwezi kuziona au kuzihisi, na mara chache
18/01/2024
17/01/2024
Kuumia kabla ya kuzaliwa* . Kabla ya kuzaliwa, watoto huweza kuumia ubongo kwa sababu k**a ya maambukizi kutoka kwa mama, lishe duni au kukosa oksijeni ya kutosha. Kuumia huku kwa ubongo kunaweza kusababisha kifafa.
Pamoja na hatari nyingine nyingi zinazoweza kumpata mtu mwenye kifafa, yafuatayo yaweza pia yakatokea:
*Status epilepticus* . Ni hali ambayo inamwathiri mtu ambaye anashikwa na kifafa mara kwa mara na kwa muda mrefu unaozidi dakika tano au k**a anashikwa na kifafa mara nyingi bila kupata ufahamu kamili katikati. Watu wenye hali hii wana yamkini kubwa ya kupata madhara ya kudumu kwenye ubongo au kufariki.
*Sudden unexpected death in epilepsy (SUDEP).* Watu wenye kifafa mara chache wanakuwa kwenye hatari ya kufa ghafla. Kiujumla, asilimia 1 ya watu wenye kifafa hufa kwa SUDEP.
*🌍🧑💻HATUA ZA KUCHUKUA KUMSAIDIA MTU ALIESHIKWA NA KIFAFA*
✍️Ukimwona mtu ameshikwa na kifafa akirusha viungo vyake ovyo na/au kupoteza ufahammu, unashauriwa kufanya yafuatayo kumsaidia:
*1️⃣* . 💁Mgeuze mwathirika alale kiubavu ili asizibwe pumzi na matapishi au maji maji mengine
*2️⃣* . 💁Weka kitu laini chini ya kichwa chake (k**a mto)
*3️⃣* . 💁Legeza nguo na vitu vingine vinavyombana mwilini au shingoni
*4️⃣* . 💁Acha eneo la wazi kumzunguka ili apate hewa ya kutosha
*5️⃣* . 💁Usimzuie kutembea labda tu kukiwa na hatari mbele yake
*6️⃣* . 💁Usiweke cho chote kinywani mwake, hata dawa au maji. Vitu hivi vyaweza kumletea madhara ya kuziba pumzi, au kujiumiza taya, ulimi, meno.
*7️⃣* . 💁Ondoa vitu vyote vyenye ncha kali ambavyo mwathirika anaweza kuviangukia akiwa ameshikwa na kifafa
*8️⃣* . 🙏Kaa na mwathirika, Usimkimbie hadi arudiwe na fahamu
17/01/2024
*Chanzo Cha Kifafa Ni Nini?*
Kifafa ni tatizo linaloweza kuwa na vyanzo vingi. Kitu cho chote kitakachovuruga mtiririko wa kawaida wa ufanyaji kazi wa neuron – kuanzia ugonjwa, uharibifu wa ubongo hadi dosari katika ukuaji wa ubongo – kinaweza kusababisha kifafa.
✍️Kifafa kinaweza kutokea kwa sababu ya dosari za usokotwaji wa ubongo, kutokuwepo uwiano baina ya kemikali ziitwazo neurotransmitters, au mchanganyiko wa haya mawili.
Wanasayansi wanaamini kuwa baadhi ya watu wenye kifafa wana viwango vikubwa sana vya excitatory neurotransmitters ambacho huongeza shughuli za neurons, wakati wengine wana viwango vidogo mno vya inhibitory neurotransmitters ambazo hupunguza shughuli za neurons kwenye ubongo. Hali hizi zote zinaweza kusababisha kuongezeka kwa shughuli za neurons na kusababisha kifafa.
Wakati mwingine ubongo hujaribu kujikarabati baada ya maumivu ya kichwa, kiharusi au tatizo jingine linaweza kwa bahati mbaya kusababisha miunganiko isiyo sahihi ya neva ambayo itasababisha kifafa. Usokotwaji wa ubongo usio sahihi unaotokea wakati wa ukuaji wa ubongo unaweza pia kuvuruga shughuli za neuron na kusababisha kifafa.
*💁Sababu za kiurithi.* Kifafa ambacho kinajitambulisha kwa jinsi kinavyotokea, au kwa eneo la ubongo linaloathirika, huonekana kwenye familia fulani. Kwa jinsi hiyo, kinaonekana kuwa ni cha urithi.
*💁Kuumia Kwa Kichwa* . Kuumia kichwa k**a kwa ajali ya gari au ajali nyingine kunaweza kusababisha kifafa.
*💁Hali ya ubongo.* Vitu vinavyoweza kuleta madhara kwenye ubongo, k**a uvimbe ndani ya ubongo au kiharusi, vinaweza kisababisha kifafa. Kiharusi kinaongoza k**a chanzo cha kifafa kwa watu wazimu wa umri wa zaidi ya miaka 35.
*💁Magonjwa ya kuambukiza.* Magonjwa ya kuambikiza k**a homa ya uti wa mgongo (meningitis), UKIMWI na viral encephalitis, yanaweza kusababisha kifafa.
*💁Kuumia kabla ya kuzaliwa* . Kabla ya kuzaliwa, watoto huweza kuumia ubongo kwa sababu k**a ya maambukizi kutoka kwa mama, lishe duni au kukosa oksijeni ya kutosha
17/01/2024
Dalili hutofautiana kulingana na aina ya kifafa. Kwa kawaida, mtu mwenye kifafa huona dalili zile zile kila wakati.
🧑⚕️Madaktari hugawanya kifafa katika makundi mawili, focal na generalized, wakizingatia jinsi tatizo katika ubongo linavyoanza.
*Focal Seizures*
Pale kifafa kinapotokea kutokana na dosari katika eneo moja la ubongo, tatizo hili huitwa focal (partial) seizure. Aina hii hugawanyika katika aina ndogo mbili:
*👉Focal seizures without loss* *of consciousness.*
Kifafa hiki hakimpotezei mtu fahamu. Kinaweza kubadilisha hisia au kubadili mwonekano, harufu, ladha au sauti ya vitu. Kinaweza kusababisha kiungo cha mwili kucheza chenyewe, k**a mkono au mguu, na dalili nyingine za pamoja za vitu kuchoma mwilini, kizunguzungu na vitu kuangaza.
*Focal seizures with impaired* *awareness* .
Kifafa hiki huambatana na mabadiliko katika au kupoteza ufahamu. Unaweza kuduwaa na kukosa mwitiko wa vitu vya kwenye mazingira au kufanya miondoko ya kujirudiarudia k**a kusugua mikono, kutafuna, kumeza au kutembea ukilizunguka eneo moja.
*Generalized seizures*
Kifafa kinachotokea kikihusisha maeneo yote ya ubongo huitwa generalized seizure. Kuna aina ndogo sita za kifafa cha aina hii:
*Absence seizures* .
Kifafa hiki huonekana zaidi kwa watoto na kinatambulika kwa kuduwaa na miondoko ya mwili isiyo ya kawaida k**a macho kukonyeza au kulamba midomo.
*Tonic seizures.*
Kifafa hiki husababisha kukak**aa kwa misuli. Kifafa hiki kwa kawaida huathiri misuli ya mgongoni, mikono na miguu na huweza kusababisha uanguke ardhini.
*Atonic seizures* .
Kifafa hiki hukusababishia ukose udhibiti wa misuli hali ambayo huweza kukufanya uzirai au uanguke.
*Clonic seizures.*
Hii huamabatana na kucheza kwa misuli kunakojirudiarudia kwa mpango.
*Myoclonic seizures* .
Hii hujitokeza kwa kucheza kwa misuli ya mikono na miguu kwa ghafla na kwa muda mfupi.
*Tonic-clonic seizures* .
Kifafa hiki ndicho kinachoweza kukufanya kupoteza fahamu ghafla, kukak**aa kwa mwili
