Tamaduni Afrika News
TEMBELEA YOUTUBE CHANNEL YETU KWA HABARI ZAIDI👉https://youtube.com/@tamaduniafricannews0011?si=1zdmd43OR-FCyMB1
31/05/2026
Bwawa la Umeme la (Barrages de la Ruzizi)
🛑.Bwawa la Ruzizi liko kwenye Mto Ruzizi, mto unaotoka katika Ziwa Kivu na kuingia katika Ziwa Tanganyika. Mto huu ni muhimu sana kwa uzalishaji wa umeme kwa nchi za , na .
🛑.Ruzizi I
Kituo cha kwanza cha umeme, kinachojulikana k**a Ruzizi I, kilijengwa miaka ya 1950 karibu na Bukavu. Kilianza kuzalisha umeme mwaka 1958 na kilikuwa mojawapo ya miradi ya kwanza mikubwa ya umeme katika eneo la Maziwa Makuu.
🛑.Ruzizi II
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme, Ruzizi II ilijengwa baadaye na kuanza kufanya kazi mwaka 1989. Kituo hiki kiliongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa nchi tatu zinazoshirikiana katika mradi huo.
🛑.Ruzizi III
Mradi wa Ruzizi III umepangwa kujengwa kati ya Ruzizi I na Ruzizi II. Lengo lake ni kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kiasi kikubwa na kusaidia maendeleo ya kiuchumi katika eneo lote la Maziwa Makuu.
🛑.Umuhimu wa Bwawa la Ruzizi
👉Huzalisha umeme kwa DRC, Rwanda na Burundi.
👉Huchangia maendeleo ya viwanda na biashara.
👉Husaidia upatikanaji wa umeme kwa mamilioni ya wananchi.
👉Ni mfano wa ushirikiano wa kikanda kati ya nchi tatu.
🛑.Kwa wakazi wa , , na maeneo mengine ya karibu, miradi ya Ruzizi imekuwa chanzo muhimu cha nishati kwa miongo kadhaa.
🛑.Bwawa za umeme za Ruzizi zina uwezo tofauti wa kuzalisha umeme:
👉Ruzizi I (Takribani 29.8 MW)
👉Ruzizi II (Takribani 43.8 MW)
👉Ruzizi III (inaendelea kupangwa/kujengwa Takribani 206 MW)
👉Ruzizi IV (mradi wa baadaye Takribani 287 MW (imepangwa)
🛑.Kwa sasa, Ruzizi I na Ruzizi II ndizo zinazofanya kazi na kwa pamoja zina uwezo wa karibu 73.6 MW.
Hata hivyo, kutokana na uchakavu wa vifaa na matatizo ya kiufundi, mara nyingi huzalisha chini ya uwezo wake kamili. Baadhi ya taarifa zinaonyesha Ruzizi I huzalisha wastani wa karibu 16–21 MW, na Ruzizi II karibu 25 MW katika vipindi fulani.
🛑.Asante🙏 kwaku Fatilia Tamaduni Afrika News. Ungependelea Tukuletee Historia ya Tukio gani, ao Mji na Eneo gani ?? Tuambie kwenye Commentaires.
Hello 👋 BUKAVU ❤️
30/05/2026
Mpaka wa , na
🛑. Kavimvira-Gatumba inaonganisha na una historia ndefu inayohusiana na ukoloni, biashara, na mahusiano ya watu wa eneo la maziwa makuu ya Afrika.
🛑🌍.Historia ya mwanzo: Kabla ya mipaka ya kisasa Wakazi wa maeneo ya na walikuwa wakivuka kwa urahisi Kulikuwa na biashara ya:
👉Samaki kutoka Lake Tanganyika
👉Chumvi
👉Mazao ya kilimo
👉Mifugo
Watu wa pande zote mbili walikuwa na uhusiano wa kifamilia na kijamii kabla ya kuwekwa kwa mpaka rasmi.
🛑⚔️.Kipindi cha ukoloni:
Upande wa ulikuwa chini ya utawala wa Belgium k**a Belgian Congo na upande wa pia ilitawaliwa kwanza na Germany, baadaye Belgium.
🛑⚔️.Wabelgiji waliweka mpaka rasmi kati ya maeneo haya Kavimvira na Gatumba zikaanza kuwa sehemu ya kudhibiti watu na bidhaa.
🛑😊.Baada ya Uhuru: Baada ya Congo kupata uhuru mwaka 1960 na Burundi kupata uhuru mwaka 1962
Mpaka huu ukawa njia muhimu kwa:
👉Biashara
👉Njia ya usafiri wa wananchi
👉Sehemu ya kuingia wakimbizi wakati wa migogoro ya Vita na Kisiasa katika eneo la Maziwa makuu ( Grands Lacs).
🛑.Asante🙏 kwaku Fatilia Tamaduni Afrika News. Ungependelea Tukuletee Historia ya Tukio gani, ao Mji na Eneo gani ?? Tuambie kwenye Commentaires.
Nina Miaka 10 natumika kazi ya Uvuvi kutana na Kijana mpambanaji aelezea changamoto ya kazi yake ya Uvuvi Mjini . Full Video ipo Youtube 👇👇
https://youtu.be/zE3V2wqphBs?si=DKmEbU_7i0x0hlY3
29/05/2026
“Challenge ya leo 😄👇
Hii ndio ilikuwa nyumba ya mwaka wa 1979.
Hakukuwa na sofa za kifahari, TV kubwa wala simu za gharama… lakini familia ilikuwa pamoja na furaha ilikuwepo ❤️
Je, kwa maoni yako maisha ya zamani yalikuwa bora kuliko ya sasa? 🤔
Tuambie kwenye commentaires 👇
29/05/2026
Mateso yakikoloni ya kwa Wakongomani
🛑.Wakati wa ukoloni katika eneo la sasa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wananchi wa Kongo walipitia mateso mengi, hasa wakati wa utawala wa Leopold II (1885–1908) na baadaye chini ya ukoloni wa Ubelgiji.
Baadhi ya mateso makubwa ni:
👉Kazi za kulazimishwa
👉Wakazi walilazimishwa kukusanya mpira (rubber) na pembe za ndovu bila malipo ya haki.
👉Waliokataa au kushindwa kutimiza kiwango walipigwa, kufungwa au kuuawa.
👉Adhabu kali
👉Askari wa kikoloni walitumia viboko na mateso mengine makali.
👉Watu walikatwa mikono k**a adhabu ya kutotimiza kazi au k**a njia ya kutisha wengine.
🛑.Kuporwa ardhi na mali:
Ardhi nyingi zilichukuliwa na serikali ya kikoloni au makampuni ya Ulaya.
👉Jamii za wenyeji zilipoteza uhuru wa kutumia rasilimali zao.
👉Mauaji na vifo vya watu wengi
👉Njaa, magonjwa, kazi ngumu na ukatili vilisababisha vifo vya mamilioni ya watu katika kipindi cha utawala wa Leopold II.
🛑.Ubaguzi
Waafrika walinyimwa haki nyingi za kisiasa, elimu ya juu na nafasi za uongozi.
Wazungu walikuwa na mamlaka makubwa kuliko wenyeji.
Kuvunjwa kwa tamaduni za jadi
Baadhi ya mila na mifumo ya utawala wa jadi ilidhoofishwa au kubadilishwa na utawala wa kikoloni.
🛑.Je! Leopold 2 ni nani? :
Leopold II alizaliwa tarehe 9 Aprili 1835 mjini na alikuwa mfalme wa Ubelgiji kuanzia mwaka 1865.
Anajulikana zaidi kwa kuanzisha na kumiliki , eneo kubwa lililokuwa katika ya leo. Tofauti na makoloni mengi ya wakati huo, Congo Free State haikuwa mali ya serikali ya Ubelgiji mwanzoni, bali mali binafsi ya Leopold II.
🛑.Jinsi alivyopata Kongo:
Katika Mkutano wa Berlin, mataifa ya Ulaya yaligawana maeneo mengi ya Afrika. Leopold II alipata utambuzi wa kimataifa wa kumiliki Congo Free State kwa madai kwamba angeendeleza biashara na kupambana na biashara ya watumwa.
🛑.Utawala wake Kongo Wakati wa utawala wake:
Watu walilazimishwa kukusanya mpira (rubber) na bidhaa nyingine.
Askari wa kikoloni walitumia adhabu kali dhidi ya waliokataa au kushindwa kutimiza malengo ya uzalishaji.
Vijiji vilichomwa na baadhi ya watu waliuawa au kujeruhiwa katika kampeni za kulazimisha kazi.
Njaa, magonjwa na kazi ngumu vilisababisha vifo vya watu wengi.😭😭.
🛑.Kutokana na taarifa za ukatili huo, viongozi wa dini, wanaharakati na waandishi wa habari kutoka Ulaya na Marekani walikosoa utawala wake.
🛑.Mwisho wa utawala wake Kongo:
Mwaka 1908, baada ya shinikizo kubwa la kimataifa, serikali ya ilichukua usimamizi wa Kongo kutoka kwa Leopold II. Eneo hilo likawa .
🛑💀.Kifo chake:
Leopold II alifariki tarehe 17 Desemba 1909 huko Laeken akiwa na umri wa miaka 74.
Leo, Leopold II anabaki kuwa mmoja wa viongozi wenye utata mkubwa katika historia ya Afrika na Congo kwa sababu ya nafasi yake katika ukoloni wa Kongo na mateso yaliyowapata Wakongomani wakati wa utawala wake.
NB: Kwanini wizara ya Elimu ya Congo haifundishi Wanafunzi Shuleni Historia ya mateso walio pitia ma Babu zetu kuteswa, kukatwa mikono, kuawa, kuporwa mali zetu etc.. ili kizazi cha Kongo kiwe nauchungu wa Taifa Lao na kupambania haki ya wananchi zidi ya Mabepari, Asante 🙏.
🛑.Asante🙏 kwaku Fatilia Tamaduni Afrika News. Ungependelea Tukuletee Historia ya Kitu gani, ao Mji na Eneo gani ?? Tuambie kwenye Comments.
28/05/2026
Hôpital Général de Référence de
🛑. Hospital ya Lemera ni moja ya hospitali muhimu sana katika jimbo la Sud-Kivu mashariki mwa . Hospitali hiyo iko katika eneo la Lemera, territoire ya , Sud-kivu eneo la Bafuliiru. Ilijengwa rasmi mwaka 1971 chini ya usimamizi wa kanisa la (Communauté des Églises de Pentecôte en Afrique Centrale).
🛑🏥.Mwanzo wa hospitali ya Lemera:
Historia yake inaanza tangu miaka ya 1920 wakati wamisionari wa Kiswidi na Kinorwe walipowasili Uvira na maeneo ya Kivu kwa kazi za dini na afya. Mwanzoni walikuwa wanatoa huduma ndogo za matibabu katika nyumba na vituo vidogo. Kadiri wagonjwa walivyoongezeka, walijenga zahanati na baadaye huduma za uzazi.
🛑.Mwaka 1971 ndipo hospitali kubwa ya Lemera ilipoanzishwa rasmi. Ilikuwa hospitali ya rufaa kwa watu wengi wa , hasa Uvira, Lemera, na vijiji vya Bafuliiru.
🛑💉.Huduma zilizokuwa zikitolewa Hospitali hiyo ilijulikana kwa:
👉Huduma za uzazi na upasuaji
👉Matibabu ya watoto
👉Tiba ya malaria, homa ya matumbo, na utapiamlo
👉Maabara, radiografia, na huduma za dharura
Wanawake wengi walikuwa wakitembea umbali mrefu kuja kujifungulia hapo kwa sababu hospitali ilikuwa na madaktari na vifaa bora kuliko vituo vingine vya vijijini.
🛑🩺.Dr. na Lemera:
Denis Mukwege alianza kufanya kazi Lemera baada ya kuhitimu udaktari Burundi. Baadaye alisomea uzazi na magonjwa ya wanawake nchini Ufaransa, kisha akarudi Lemera mwaka 1989. Mwaka 1992 akawa mkurugenzi wa hospitali hiyo. Alisaidia sana wanawake waliokuwa wanapata matatizo wakati wa kujifungua na alifanya upasuaji mwingi wa kuokoa maisha ya kina mama.
🛑😭.Mauaji ya Lemera mwaka 1996
Wakati Vita vya Kwanza vya Congo vilipoanza mwaka 1996, hospitali ya Lemera ilivamiwa tarehe 6 Oktoba 1996 na waasi wa walioungwa mkono na na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.
Wagonjwa, wauguzi, na baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakitibiwa waliuawa ndani ya hospitali. Ripoti ya UN Mapping ilitaja watu karibu 37 kuuawa, baadhi yao wakiwa vitandani mwa wagonjwa. Hospitali iliharibiwa na kuporwa vifaa vya tiba😭😭.
Tukio hilo linajulikana k**a “ ” na linaendelea kukumbukwa k**a moja ya mashambulizi mabaya dhidi ya hospitali katika historia ya vita vya Congo.😭
🛑.Baada ya vita: Baada ya uharibifu huo, hospitali ilijengwa tena kwa msaada wa mashirika ya kimataifa na makanisa. Leo bado inaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa Sud-Kivu, ingawa imepitia changamoto nyingi za vita na ukosefu wa vifaa.
🛑🏥.Uhusiano wake na Hospitali ya :
Baada ya Lemera kuharibiwa, Dr. Mukwege alihamia Bukavu na kuanzisha Hôpital de Panzi mwaka 1999. Ndiyo maana watu wengi husema kuwa “roho ya Lemera iliendelea Panzi,” kwa sababu uzoefu na kazi ya kusaidia wanawake ilihamia huko.
🛑.Asante🙏 kwaku Fatilia Tamaduni Afrika News. Ungependelea Tukuletee Historia ya Kitu gani, ao Mji na Eneo gani ?? Tuambie kwenye Comments.
27/05/2026
Eid Uvira sheikh mkorea Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.
Mtazamo WA Siku ya Eid Mjini Uvira.
Katazame video nzima kwenye Channel yetu ya YouTube 👇👇 https://youtube.com/?si=-moNQq8oi8nuV6Gh
Click here to claim your Sponsored Listing.

30/05/2026